Pages

table

table

Sunday, May 13, 2018

NJIA RAHISI YA KUSAFISHA TUMBO




Kusafisha tumbo (Colon Flush/cleanse) ni njia itumikayo kuondoa masalia ya uchafu uliorundikana katika utumbo mkubwa, licha ya kwamba unaweza kuwa unapata choo vizuri lakini tambua yapo mabaki ya uchafu yanayobakia. Kuendelea kubakia kwa mabaki hayo inaelezwa ndio chanzo kikuu cha mazalia ya bakteria waletao maradhi mwilini. Inashauriwa kufanya Colon Cleanse/ Flush mara moja moja ili kuondoa mabaki hayo tumboni. Aidha zipo faida mbalimbali zinazopatikana pindi unaposafisha tumbo faida mojawapo ni kurudisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika hali nzuri.Hapo zama za kale zilikuwepo njia kadhaa zilizokuwa zikitumika kukamilisha tiba hii na hadi sasa zimegundulika njia lukuki zikiwemo dawa mahususi za hosptali na pia zipo njia rahisi unazoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa nyumbani. Ifuatayo ni njia nyepesi na yenye matokea chanya kwa asilimia mia moja na isiyo na madhara kiafya ya jinsi ya kujisafisha tumbo ili kuondoa uchafu uliorundikana tumboni.


 



                                                   




Matumizi
chemsha maji yawe ya uvugu uvugu ( Yasiwe ya moto ) kiasi cha glasi moja ujazo wa mililita 400 kisha tia vijiko viwili vidogo vya chumvi ( hakikisha chumvi hii inakuwa ni chumvi ya mawe ( sea salt ) isiyo na iodine)  changanya hadi chumvi hiyo iyeyuke kabisa kisha kamulia vipande viwili vya ndimu na unywe mchanganyiko huo asubuhi kabla ujala kitu chochote. Mchanganyiko huu huanza kufanya kazi ndani ya dakika 10 hadi 15 unaweza pata choo mara 2 hadi 3 au zaidi kulingana na uchafu ulionao. Baada ya kumaliza kuflashi kula matunda freshi kwa wingi. Zingatia mfumo mzuri wa ulaji na unywaji maji kwa kiwango kinachotakiwa ili kuendelea kuweka tumbo lako katika hali nzuri baada ya kulisafisha, ulaji mbaya na unywaji mdogo wa maji utapelekea uchafu kurundikana kwa haraka zaidi.


Thursday, May 3, 2018

TIBA YA BAWASIRI


Bawasiri ni kijinyama kinachotokea ndani au nje ya njia ya haja kubwa chenye maumivu makali sana unapokwenda kujisaidia na wakati mwingine kushindwa kukaa vizuri kwenye kiti. Ni moja  kati ya Ugonjwa unaosumbua wengi hivi sasa, wapo watu ambao hufanya siri wapatapo ugonjwa huu na kuishia kuugulia maumivu makali wakiwa wamejifungia ndani, kuna aina mbili za bawasiri            ( Bawasiri ya ndani na nje ) Zipo sababu nyingi zinazopelekea kupata ugonjwa huu, moja ya sababu ni unywaji hafifu wa maji na matunda ili kusadia mfumo wa usagaji chakula hali ianayopelekea muathirika kupata choo kigumu au kukosa kwa muda mrefu na  kutumia nguvu kubwa anapojisaidia na kusababisha misuli ya haja kubwa kuvimba kutokana na pressure hiyo, sababu ingine ni kuhara kwa muda mrefu. Ugonjwa huu ni wenye kujirudia rudi mara kwa mara kutokana na tabia ya ulaji wako, zingatia ulaji bora ili kujiepeusha na hali hi.Hakuna Ugonjwa usio na dawa, nini cha kufanya pindi upatapo hali hii?

Jinsi ya kujitibu
Pakaa maji maji ya alovera kwenye kijiuvimbe asubuhi, mchana na jioni na uwe unakula asali iliyo changanywa na habatsoda kijiko kimoja kila siku asubuhi kabla ujala kitu chochote, au kunywa chai iliyochangaywa habat soda na binzari nyembamba asubuhi kabla ujala kitu chochote kwa muda wa siku 14 uvimbe utaondoka kabisa shaka ondoa. Pia unaweza kutumia mafuta ya mnyonyo kupakaa kwenye uvimbe kama utakosa  mualovera, hakikisha unakula chungwa moja pamoja na maganda yake katika kila mlo ili kusaidia usagaji wa chakula mpaka utakapo pona. 

 
 
Binzari nyembamba

Monday, April 16, 2018

DAWA SUGU YA UTI


Urinary tract infection (U.T.I) ni ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe kama bakteria, fangasi na virus. Mara nyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili,Wakati mwingine bakteria wanaweza zidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo. U.T.I's inaweza kuathiri njia ya haja ndogo, kibofu cha mkojo na figo.Tafiti zinaonyesha Wanawake ndio wathirika zaidi wa ugonjwa huu.

Njia mbadala ya kujiking na UTI
Zipo njia kadhaa ambazo zimeshauriwa na wana tiba ikiwa ni pamoja na unywaji wa maji mengi, usafi wa mara kwa mara wa choo na wanawake kujisafisha kila wajisaidiapo haja ndogo kwa kutumia maji safi na salama wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele kurudi nyuma ili kulinda urethra. Lakini wapo watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huu licha ya kutumia njia zote zilizoshauriwa kitaalam. Nini tiba ya UTI sugu?

BICARBONATE OF SODA






Ndio Bicarbonate of Soda wengi wanaitambua kama chapa simba ndio suluhisho lako sasa, sodium corbonate iliyomo kwenye unga huo ina aminika kuwa na uwezo wa kufanya kazi mbalimbali kwa matumizi lukiki katika kila siku ya maisha yetu ikiwemo kung’arisha  meno, vyombo nk ikiwa na faida za kiafya pia.
Matumizi
Chukua unga wa Bicarboante soda robo kijiko cha chai changanya kwenye glasi ya maji yenye ujazo wa mililita 400 kisha uwe una kunywa asubuhi kabla ya ujala kitu chochote na jioni kwa siku 7 utapona kabisa.



Sunday, April 15, 2018

KISUKARI (DIABETES)

Kisukari (Diabetes) moja kati ya mogonjwa yaliyoibuka miaka ya hivi karibuni, ugonjwa huu mwanzoni uliaminika huwapata wazee tu na vijana wa makamo lakini hivi sasa takwimu zinaonyesha ni ugonjwa unaowapata hata watoto kuanzia umri wa miaka 4 na kuendelea hakika ni hatari isiyoweza kusimulika.Kiini cha tatizo hili inasemekana ni ulaji uliopindukia wa vyakula vyenye sukari nyingi na wanga ( soda, mikate nk) vyakula ambavyo upelekea insulin kushindwa kusambaza sukari hiyo mwilini kutokana na uwingi unaopokea kutoka kwa mlaji, sababu ingine ni mfumo wa maisha wa watu wengi kutopendelea kufanya mazoezi ili kupunguza sukari inayoingia mwilini. nini tiba ya kisukari au kinga yake?

Rose Periwinkle




Haya ni maua common kabisa nyumbani kama hauna kwako basi yapo kwa jirani, ua hili ni moja ya kati ya tiba bora kabisa ya ugonjwa wa kisukari kama ulikuwa ufahamu hili tambua sasa.

Matumizi
Tafuna jani la ua hili kutwa mara tatu, asubuhi moja, mchana na jioni kwa siku 14 hadi 21 kwa aina zote za kisukari ( Type1 na 2) au chuma majani 12 hadi 14 kisha tengeneza juisi na unywe glass 1 kutwa mara tatu. Pia ni kinga kwa wale ambao bado ugonjwa huu haujakupata tafuna jani moja atleast mara moja kwa wiki au mbili.



Hibiscus FLowers

                     

  


Nani asiyelijua ua hili?  Ni maua tunayokutana nayo kila siku ya maisha yetu, ni moja kati ya tiba ya kisukari kuaznia siku 8 hadi 28 na unapona kabisa kisukari hakuna miujiza katika hili. 


Matumizi 

Chuma majani ya ua hili kuanzia majani 10 hadi 12 na yasage kwa kutumia blenda au kinu kisha changanya maji lita 1 unywe asubuhi 1 na jioni glasi 1 kwa siku 8 hadi siku 28 kulingana na usugu wa ugonjwa ulionao.Kabla ya kutumia chukua kiwango cha sukari na uwe unapima kiwango hicho kila ukamilishapo muda wa dozi ili kujua km umepona au la muda wa dozi ni kuanzia siku 8 hadi 28.  

Sunday, August 28, 2016

MATUMIZI YA DAWA ZA MENO NA MADHARA YA KIAFYA KWA MTUMIAJI

Tambua dawa ya meno zinavyotengenezwa ili kuepusha madhara ya kimwili unayoweza kuyapata hasa kwa watoto wadogo, epusha kumpigisha mtoto mdogo mswaki kwa kutumia dawa ya meno, ni mara nyingi watoto upendelea kumeza kwa radha zake wakifikiri ni ice cream au juice  aidha kwa makusudi au kwa kutokujua. Dawa hizo nyingi zimetengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa kemikali kali .

Kabla ujanunua dawa ya meno angalia lebo ya rangi yake kama inavyoonekana pichani ili kujiepusha kununua dawa zenye Kemikali nyingi zitakazo kuletea madhara makubwa kiafya.

Ni vizuri ukanunua dawa yenye lebo ya kijani kwa matumizi yako na familia kiujumla, dawa hizi zimetengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa asili wa mimea, sio dawa zote zilizoandikwa herbal zimetengezwa kwa kutumia mimea asili, ndio maana watengenezaji wamelazimishwa kuweka lebo hizi ili kuwajuisha watumiaji wake. Swali la kujiuliza ni kwamba

je ni mwenye kiwanda gani anayetoa elimu hii kwa watumiaji wa dawa hizi, au wapi ulishawahi kupata elimu hii?



Saturday, August 20, 2016

TIBA YA SARATANI (CANCER)

HABALSODA

Paka mafuta ya habalsoda mara tatu kila siku pamoja na kula kijiko cha unga cha unga wake kila umalizapo kula katika kikombe cha juice ya karoti.Endelea kufanya hivyo kwa muda wa miezi mitatu. 



STAFELI 

Pia pendelea kunywa juisi ya tunda la mtopetope au stafeli, Stafeli lina mchanganyiko wa virutubisho wenye uwezo mkubwa wa kuthibiti ukuwaji wa seli  za saratan mara 10,000 zaidi ya dawa ya adriamycin ambayo ndio hutumika kutibu saratani. 

MAJANI YA MSTAFELI

Licha ya tunda la mstafeli 10,000  kuwa na virutubisho vyenye uwezo mkubwa wa kuthibiti ukuwaji wa seli za saratani, utafiti umeonyesha majani yake pia yana uwezo sawa na tunda hilo.Tumia majani hayo kwa kutengeneza juice na uinywe au tafuta jani moja la mstafeli kutwa mara tatu pia unaweza kuchuma majani hayo na kuyakausha kwa matumizi ya vinywaji vya moto kama chai na vingine unaweza  kutumia kama tiba au kinga ya saratani zote.Utafini umeonyesha majani ya stafeli yanauwezo wa kutibu aina 12 za saratani zikiwemo saratani ya matiti na tezi dume, tumia majani haya 100% utapona kabisa.




ASALI 
Chukua mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligarmu 100 kila wiki mara moja na kula asali pamoja na nta yake kila siku kiasi cha kikombe kimoja na sugua mwili wako kwa asali na mafuta ya habalsoda, kisha oga baada ya saa moja kwa maji yenye uvuguuvugu, baadae kula asali iliyochanganywa na unga wa habalsoda katika juisi ya karoti kila siku.






                



KITUNGUU SAUMU

Kitunguusaumu kina virutubisho vingi vinavyozuia saratani, kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu saumu na karoti kwa wingi. Kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu tiba hii itampa mgonjwa matokeo mazuri kwa haraka.


                     

KITUNGUU MAJI
Kausha vizuri maganda ya kitunguu kweye jua, yasage na kiasi kama hichi cha magamba ya Muoka halafu yakande katika asali, chukua kiasi cha kijiko kimoja ukoroge katika juisi ya karoti na unywe kila siku kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo..Baada ya hapo utakuwa ukivuta puani moshi wa kitunguu kabla ya kulala kwa muda wa mwezi mmoja.