Kusafisha
tumbo (Colon Flush/cleanse) ni njia itumikayo kuondoa masalia ya uchafu
uliorundikana katika utumbo mkubwa, licha ya kwamba unaweza kuwa unapata choo
vizuri lakini tambua yapo mabaki ya uchafu yanayobakia. Kuendelea kubakia kwa
mabaki hayo inaelezwa ndio chanzo kikuu cha mazalia ya bakteria waletao maradhi
mwilini. Inashauriwa kufanya Colon Cleanse/ Flush mara moja moja ili kuondoa
mabaki hayo tumboni. Aidha zipo faida mbalimbali zinazopatikana pindi
unaposafisha tumbo faida mojawapo ni kurudisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
katika hali nzuri.Hapo zama za kale zilikuwepo njia kadhaa zilizokuwa
zikitumika kukamilisha tiba hii na hadi sasa zimegundulika njia lukuki zikiwemo
dawa mahususi za hosptali na pia zipo njia rahisi unazoweza kufanya wewe
mwenyewe ukiwa nyumbani. Ifuatayo ni njia nyepesi na yenye matokea chanya kwa
asilimia mia moja na isiyo na madhara kiafya ya jinsi ya kujisafisha tumbo ili
kuondoa uchafu uliorundikana tumboni.
Matumizi
chemsha maji yawe ya uvugu uvugu ( Yasiwe ya moto ) kiasi cha glasi moja ujazo wa mililita 400 kisha tia vijiko viwili vidogo vya chumvi ( hakikisha chumvi hii inakuwa ni chumvi ya mawe ( sea salt ) isiyo na iodine) changanya hadi chumvi hiyo iyeyuke kabisa kisha kamulia vipande viwili vya ndimu na unywe mchanganyiko huo asubuhi kabla ujala kitu chochote. Mchanganyiko huu huanza kufanya kazi ndani ya dakika 10 hadi 15 unaweza pata choo mara 2 hadi 3 au zaidi kulingana na uchafu ulionao. Baada ya kumaliza kuflashi kula matunda freshi kwa wingi. Zingatia mfumo mzuri wa ulaji na unywaji maji kwa kiwango kinachotakiwa ili kuendelea kuweka tumbo lako katika hali nzuri baada ya kulisafisha, ulaji mbaya na unywaji mdogo wa maji utapelekea uchafu kurundikana kwa haraka zaidi.
No comments:
Post a Comment