Pages

table

table

Thursday, May 3, 2018

TIBA YA BAWASIRI


Bawasiri ni kijinyama kinachotokea ndani au nje ya njia ya haja kubwa chenye maumivu makali sana unapokwenda kujisaidia na wakati mwingine kushindwa kukaa vizuri kwenye kiti. Ni moja  kati ya Ugonjwa unaosumbua wengi hivi sasa, wapo watu ambao hufanya siri wapatapo ugonjwa huu na kuishia kuugulia maumivu makali wakiwa wamejifungia ndani, kuna aina mbili za bawasiri            ( Bawasiri ya ndani na nje ) Zipo sababu nyingi zinazopelekea kupata ugonjwa huu, moja ya sababu ni unywaji hafifu wa maji na matunda ili kusadia mfumo wa usagaji chakula hali ianayopelekea muathirika kupata choo kigumu au kukosa kwa muda mrefu na  kutumia nguvu kubwa anapojisaidia na kusababisha misuli ya haja kubwa kuvimba kutokana na pressure hiyo, sababu ingine ni kuhara kwa muda mrefu. Ugonjwa huu ni wenye kujirudia rudi mara kwa mara kutokana na tabia ya ulaji wako, zingatia ulaji bora ili kujiepeusha na hali hi.Hakuna Ugonjwa usio na dawa, nini cha kufanya pindi upatapo hali hii?

Jinsi ya kujitibu
Pakaa maji maji ya alovera kwenye kijiuvimbe asubuhi, mchana na jioni na uwe unakula asali iliyo changanywa na habatsoda kijiko kimoja kila siku asubuhi kabla ujala kitu chochote, au kunywa chai iliyochangaywa habat soda na binzari nyembamba asubuhi kabla ujala kitu chochote kwa muda wa siku 14 uvimbe utaondoka kabisa shaka ondoa. Pia unaweza kutumia mafuta ya mnyonyo kupakaa kwenye uvimbe kama utakosa  mualovera, hakikisha unakula chungwa moja pamoja na maganda yake katika kila mlo ili kusaidia usagaji wa chakula mpaka utakapo pona. 

 
 
Binzari nyembamba

No comments:

Post a Comment