Pages

table

table

Thursday, August 18, 2016

KUPUNGUZA UZITO (WEIGHT LOSS)


 

Tatizo la Uzito kwasasa linawakumba wakubwa na watoto, tatizo hili chanzo chake ni ulaji mbaya na aina ya vyakula vinavyopendelewa kuliwa na wengi km vile chips, chocolate, vyakula vyenye mafuta, na vyakula vilivyosindikwa viwandani.Hali hii inapelekea watu wengi kuongezeka uzito kwa haraka, wengi wanajitahidi kurudi katika hali zao za awali kwa kutumia kila aina ya njia zikiwemo kunywa madawa ya kutoa mafuta, Mazoezi makali na hata operation kwa kuondoa mafuta yalioganda mwilini.

Njia rahisi ya kupunguza uzito, kuyeyusha mafuta mwilini na kumaliza vitambi na kufurahia mwili wako wa awali kwa Wanaume na Wanawake tiba yake ni kufanya yafuatayo:-

1. Kila siku kunywa maji ya kitunguumaji kiasi cha kijiko kidogo, unaweza kuchanganya juisi hiyo na aina ya juisi ya matunda yoyote ile uipendayo, juisi iwe ni ya kusaga mwenyewe. Juisi hii inauwezo wa kupunguza uzito na kuyeyusha mafuta kwa haraka sana.

                      

2. Punguza kukaa sana mahali pamoja weka mazoea ya kutembea sana ata kama una gari unashauriwa siku mbili kwa wiki kutembea kwa miguu umbali usiopungua kilomita mbili na kufanya mazoezi kwa wingi, unaweza kutenga lisaa limoja kwa mazoezi. Kama unashindwa kufanya mazoezi peke yako jiunge kwenye sport club ili kupata kampani zaidi.  


No comments:

Post a Comment